Madaktari Wauza Figo za Watu 109

Saturday, September 18, 2010 / Posted by ishak /


Madaktari watano wa nchini Afrika Kusini wamepandishwa kizimbani kwa kuuza figo za watu 109 katika kipindi cha miaka miwili.
Madaktari watano wa hospitali binafsi kubwa ya nchini Afrika Kusini wamepandishwa kizimbani kwa kuwauzia figo za watu 109 matajiri wa Israel.

Madaktari hao walifanya biashara haramu ya viungo vya binadamu kwa kununua kwa bei rahisi figo za watu maskini toka Israel, Romania na Brazil.

Madaktari hao katika kipindi cha kati ya mwaka 2001 na 2003 walizininua figo 109 na kufanya operesheni kinyume cha sheria kuwapandikiza matajiri wa Israel.

Miongoni mwa waliopandishwa kizimbani ni mkuu wa mtandao wa hospitali kubwa binafsi nchini Afrika Kusini wa Netcare bwana Richard Friedland, lilisema gazeti la The Star.

"Raia wa Israel wanaohitaji figo, waliletwa nchini Afrika Kusini kwaajili ya kupandikizwa figo za watu wengine kwenye hospitali ya St. Augustine iliyopo mjini Durban".

"Mwanzoni walikuwa wakinunua figo toka kwa raia wa Israel lakini baadae waliamua kununua figo za raia wa Brazili na Romania kwakuwa figo zao zilikuwa zikiuzwa kwa bei chee".

Figo ya raia wa Israel ilikuwa ikinunuliwa kwa dola 20,000 wakati figo za Wabrazili na Waromania zilikuwa zikinunuliwa kwa dola 6,000 tu, ilisema taarifa ya mwendesha mashtaka.

source nifahamishe