Wajukuu wa Osama Bin Laden Wafariki

Wednesday, September 15, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamama aliyekuwa amejitolea kupandikizwa mimba ya watoto mapacha wa mtoto wa kiongozi wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden, amewapoteza watoto hao baada ya mimba yake kuharibika kufuatia kichapo alichopewa mtaani na wanaume wawili ambao hawajajulikana.
Mtoto wa Osama Bina Laden, Omar Bin Laden mwenye umri wa miaka 29 ambaye amemuoa mwanamke wa Kiingereza ambaye alikuwa hana uwezo wa kupata mimba kutokana na umri wake, alimkodisha mwanamke toka mji wa Bristol nchini Uingereza abebe mimba yake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 anayejulikana kwa jina la Louise Pollard alipoteza mimba hiyo ya watoto wawili mapacha baada ya kushambuliwa na watu wawili wasiojulikana wakati akielekea nyumbani kwake toka kwenye mgahawa mmoja nchini Syria.

Louise ambaye zamani alikuwa akicheza dansi za utupu kwenye klabu za starehe nchni Uingereza, alienda hospitali ambako aliambiwa kuwa watoto wote wawili walioko tumboni mwake wamefariki.

Louise alisema kuwa hajajua sababu ya wanaume hao kumshambulia ingawa alisema kuwa watu wengi wanamfahamu kama mwanamke aliyebeba mimba ya wajukuu wa mkuu wa Al Qaeda, Osama bin Laden.

Mke wa mtoto wa Osama, Zaina mwenye umri wa miaka 54, ambaye awali alikuwa akijulikana kama Jane Felix-Browne alisema kuwa Omar amekumbwa na upungufu wa akili hivyo wameamua kuachana.

Omar na Zaina walipanga kumlipa paundi 10,000 mwanamke huyo baada ya kujifungua watoto hao mapacha.

source nifahamishe