Amuua Mkewe Na Kisha Kuila Maiti Yake

Monday, May 17, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka 15 baada ya kumuua mkewe kwa kumchoma choma na kisu mara 250 na kisha kula nyama za mapafu yake kabla ya kunywa damu yake mbele ya mtoto wake wa miaka minne.
Mohammad Solaiman alihukumiwa kwenda jela kati ya miaka 15 na kifungo cha maisha kwa kumuua kikatili mkewe Shahida Sultanna ndani ya nyumba yao mjini New York katika tukio lililotokea mwaka 2007.

Binti yao mwenye umri wa miaka minne alikuwa chumba cha pili wakati baba yake alipokuwa akimuua mama yake na alishuhudia kitendo cha baba yake akinywa damu ya mama yake.

"Alichukua maini na mapafu yake na kuyatafuna", alisema dada wa marehemu na kuongeza "Alikunywa damu yake, binti yake ameniambia".

Wakili wa Solaiman, John Scarpa alikanusha madai ya Solaiman kumgeuza asusa mkewe ingawa alikubali kumuua mkewe.

Wakili huyo aliendelea kusema kuwa Solaiman alikuwa akipigwa na kunyanywaswa sana na mkewe na hiyo ndio sababu iliyompelekea kufanya mauaji.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Richard Buchter alisema kuwa faili la mshtakiwa halikusema chochote kama alikuwa akinyanywaswa na mkewe.

"Tunachojua ni kwamba, mshtakiwa alimchoma na kisu mkewe usoni, shingoni, tumboni, mgomgoni na kwenye maeneo yake ya siri", jaji Buchter alisema.

"Kuthibitisha kitendo chake cha kikatili alimuonyesha binti yake wa miaka minne mabaki ya mwili wa mama yake", aliongeza jaji Buchter.

Solaiman alihukumiwa kwenda jela kati ya kifungo cha miaka 15 na kifungo cha maisha baada ya kukiri kufanya mauaji hayo.

source nifahamishe

Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia

Monday, May 17, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mrembo toka Michigan, Rima Fakih ameshinda mashindano ya urembo wa Marekani Miss USA 2010 na kuwa mwarabu wa kwanza kushinda mashindano hayo makubwa ya urembo nchini Marekani.
Rima Fakih Mmarekani mwenye asili ya Lebanon amekuwa Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kushinda mashindano ya Miss USA katika historia ya mashindano hayo.

Katika mashindano yaliyofanyika mjini Las Vegas na kuonyeshwa live na televisheni ya NBC, Fakih aliwafunika jumla ya warembo 50 toka majimbo mbalimbali ya Marekani na kutwaa taji la Miss USA 2010.

Fakih mwenye umri wa miaka 24, alitwaa taji la urembo wa Marekani akifuatiwa na Miss Oklahoma aliyeshika nafasi ya pili, Miss Virginia, Miss Colorado na Miss Maine.

Fakih ataiwakilisha Marekani kwenye mashindano ya urembo ya Miss Universe yatakayofanyika baadae mwaka huu.


source nifahamishe

Wanafunzi Wanyonyana Sehemu za Siri Darasani Huku Mwalimu Akichekelea

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwalimu mmoja wa nchini Marekani anafanyiwa uchunguzi baada ya kuwaachia wanafunzi wake wanyonyane sehemu za siri darasani huku wanafunzi wengine wakichukua video za tukio hilo na kupiga picha.
Televisheni ya KTLA ya Marekani imeripoti kuwa tukio hilo limetokea kwenye shule ya Haydock Intermediate School iliyopo Oxnard, California ambapo mwanafunzi wa kike na wa kiume walinyonyana sehemu za siri darasani mbele ya wanafunzi wenzao waliojaa darasani kwaajili ya kuangalia filamu iliyoandaliwa na mwalimu huyo.

Mwanafunzi wa kiume wa darasa la nane na mwanafunzi wa kike wa darasa la saba ndio waliohusika katika tukio hilo ambalo limewakasirisha wazazi wengi nchini Marekani.

Wanafunzi walichukua video za tukio hilo kwa kutumia simu zao huku wengine wakipiga picha ambapo mwalimu wao alipuuza na hakuchukua hatua yoyote ile kuzuia kitendo hicho kiovu darasani.

Mwalimu huyo amepewa likizo yenye malipo wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Wanafunzi waliofanya kitendo hicho hawajachukuliwa hatua yoyote na wanahudhuria shuleni kama kawaida.

Sylvia Ramirez, mmoja wa wazazi ambaye anafanya kazi katika mgahawa wa shule hiyo alisema kuwa ameiona video ya ngono ya wanafunzi hao.

"Inasikitisha sana kuona hawalitilii uzito suala hili, shoo ya ngono inafanyika darasani, inasikitisha sana", alisema Ramirez.

Polisi wanalifanyia uchunguzi tukio hilo baada ya kupewa taarifa.


source nifahamishe

Waislamu Walazimishwa Kula Nguruwe Ili Ziwape Nguvu

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wanawake watatu wa kiislamu toka nchini Indonesia walilazimishwa na bosi wao katika kiwanda cha nguo nchini Taiwan wale nyama ya nguruwe ili ziwape nguvu na stamina ya kufanya kazi.
Wanawake watatu wa kiislamu ambao ni raia wa Indonesia, walilazimishwa na bosi wao katika kiwanda cha nguo mjini Taipei wale nyama ya nguruwe au la mishahara yao itapunguzwa.

Kwa muda wa miezi saba wanawake hao walilazimishwa na bosi wao kula vyakula vyenye nyama ya nguruwe vilivyokuwa vikigaiwa kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho kwakuwa bosi wa kiwanda hicho alikuwa akiamini kuwa nyama ya nguruwe ingewapa nguvu na stamina ya kufanya kazi wanawake hao.

Bosi wa kiwanda cha nguo cha Shin Hua Hang Fashion Co, Chang Wen-lin amefikishwa mahakamani kwa kuwalazimisha wanawake hao wale nyama ya nguruwe katika kipindi cha ajira yao kuanzia mwezi septemba 2008 hadi April 2009.

Katika jalada la kesi aliyofunguliwa mahakamani, Cheng aliamini kuwa nyama ya
nguruwe ingewapa stamina ya kufanya kazi wanawake hao na alitishia kuwakata mishahara yao iwapo wasingekubali kula nyama hiyo.

Waendesha mashtaka wanataka Chang Wen-Lin ahukumiwe kwenda jela miezi minane.

Wanawake hao walipelekea malalamiko yao kwa taasisi ya kutetea wafanyakazi mjini Taipei ambapo walisema kuwa walifanyishwa kazi nyingi kuliko kawaida katika kipindi cha miezi minane bila ya kulipwa chochote.

Taasisi hiyo ndiyo ililifikisha suala hilo mahakamani kwa niaba ya wanawake hao ambao kutokana na hofu za masuala ya uhamiaji walikuwa wakihofia kurudishwa kwao iwapo wangemchukulia hatua bosi wao.

Wanawake hao hivi sasa wametafutiwa kazi kwenye kampuni nyingine mjini Taipei.

Kuna vibarua takribani 350,000 nchini Taiwan ambapo wengi wao wanatoka Indonesia, Philippines na Vietnam.

Katika ripoti ya mwaka 2009 ya haki za binadamu duniani, tatizo kubwa lililotajwa kuikabili Taiwan lilikuwa ni unyanyasaji wa wafanyakazi makazini.

Ripoti hiyo ilisema kuwa wafanyakazi wengi huogopa kuripoti matatizo yanayowakabili kwa kuhofia kupoteza ajira zao.

source nifahamishe

Mwanaume na Mwanamke Wabakwa Afrika Kusini

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa mjini Cape Town nchini Afrika Kusini amepandishwa kizimbani kwa kuwabaka wafanyakazi wenzake wawili, mmoja ni mwanaume na mwingine ni mwanamke.
Mwanaume aliyebakwa aliiambia mahakama ya Cape Town kuwa siku ya tukio ambayo kulikuwa na party ya wafanyakazi, alikunywa sana pombe kiasi cha kupitiwa na usingizi.

Mwanaume huyo alisema kuwa alipoamka aliona mambo hayako sawa kwenye maungo yake ya nyuma akihisi hali tofauti.

Mwanaume huyo aliendelea kusema kuwa aligundua kuwa alikuwa amelawitiwa baada ya kurudi kazini siku chache baadae na kusikia wafanyakazi wenzake wakijadili jinsi alivyofanyiwa mchezo mbaya na mwanaume mwenzake.

Mwanaume huyo aliiambia mahakama kuwa aliambiwa na mfanyakazi mwenzake aliyeshuhudia tukio hilo kuwa alimuona mfanyakazi mwenzao akijiandaa kumbaka lakini hakuchukua hatua yoyote.

Mwanaume huyo aliongeza kuwa alienda polisi ambapo alifanyiwa uchunguzi uliothibitisha kuwa aliingiliwa kinyume cha maumbile.

Mwanamke aliyebakwa ni mpenzi wa shuhuda aliyemuona mwanaume akibakwa.

Mwanamke huyo alisema kuwa mtuhumiwa alimkaba koo kwa nguvu na alipozimia mtuhumiwa alimbaka na kumuibia simu yake.

Ripoti ya daktari ilithibitisha kuwa mwanamke huyo alibakwa.

Mtuhumiwa amekanusha madai yote mawili ya ubakaji. Uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea.

source nifahamishe

Afariki Baada ya Kuona Maiti za Ajali ya Ndege

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Afisa mmoja wa Libya amefariki baada ya kuona maiti za ajali ya ndege wakati alipokimbilia kwenye eneo la tukio kutoa msaada.
Afisa huyo ambaye ni mlinzi kwenye uwanja wa ndege alifariki baada ya kuona maiti za watu 102 waliokuwemo kwenye ndege ya Libya ambayo ililipuka wakati wa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.

Taarifa zinasema kuwa mlinzi huyo alikimbilia kwenye eneo la ajali kwa nia ya kutoa msaada lakini alipofika na kuziona maiti zikiwa zimezagaa kila kona ugonjwa wake wa kisukari ulimzidia na hapo hapo aliiaga dunia.

Taarifa zaidi kuhusiana na kifo chake hazikutolewa ingawa taarifa zilisema kuwa mlinzi huyo alikuwa ni mzee.

Wakati huo huo mtu pekee aliyenusurika kwenye ajali hiyo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa, Ruben, amesafirishwa leo kurudishwa kwao Uholanzi.

Ruben alikuwa na baba yake, mama yake pamoja na kaka yake mwenye umri wa miaka 11 kwenye ndege hiyo lakini wote walifariki kwenye ajali hiyo.

Ruben na wazazi wake pamoja na kaka yake walikuwa likizo nchini Afrika Kusini kusherehekea ndoa ya wazazi wake kutimiza mwaka mmoja.

Shangazi na mjomba wake toka Uholanzi walikimbilia mjini Tripoli kuwa karibu na mtoto huyo ambaye alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha kadhaa kwenye miguu yake.

Mtoto huyo ameishaambiwa na shangazi yake kuwa wazazi wake na kaka yake wamefariki kwenye ajali hiyo mbaya ya ndege

source nifahamishe

Mshindi wa Tuzo Milionea Akabidhiwa Milioni 100 Zake

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imemkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 mshindi wa Promosheni ya Tuzo milionea Bw. Bernard John (27) mkazi wa Morogoro.
Bw. Bernard John (27) alikabidhiwa mshiko wake katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake na kuhudhuriwa na maofisa wa Vodacom ndugu jamaa na marafiki.

Ujumbe wa Vodacom Tanzania uliongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia ambaye pamoja na mambo mengine alimpongeza mshindi huyo na kumshauri azitumie fedha hizo kuboresha maisha yake.

“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania, ninapenda kuchukua fursa hii kukupongeza sana ni furaha iliyoje kuona mwenzetu katika familia kubwa ya Vodacom Tanzania yenye wateja zaidi ya milioni saba anabadilisha maisha yake kwa kuyaboresha,” alisema.

John alishinda kupitia droo kubwa iliyochezeshwa na kampuni hiyo na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha ITV chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Akiongea katika hafla hiyo, John aliishukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hiyo ambayo alisema inaboresha maisha ya wateja wa Vodacom.

“Kwakweli ninaipongeza Vodacom Tanzania kwa kuanzisha promosheni hii ambayo imebadilisha kabisa maisha yangu na kuwa yenye matumaini, nitazitumia fedha hizi kwa kujiendeleza zaidi kielimu na manufaa ya familia yangu na jamii yangu inayonizunguka,”alisema.

Promosheni ya Tuzo Milionea kwa mwaka huu, ilianza mapema mwezi Februari lengo likiwa ni kuwarejeshea wateja wa Vodacom sehemu ya kile Vodacom inachokipata na pia kuboresha maisha ya wateja wake.

Correia alifafanua kuwa tangu kuanza kwa promosheni hiyo ambayo imedumu kwa miezi mitatu sasa, wateja wa wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwa ni pamoja na muda wa maongezi.

Correia alisema kuwa kupitia Promosheni ya Tuzo Milionea, wateja Saba wa Vodacom walijishindia muda wa maongezi wenye thamani ya sh. 100,000 kupitia droo za kila wiki na hadi mwisho wa promosheni hiyo wateja wetu watajishindia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni tisa.

Aidha aliongeza kuwa Promosheni hii ni mwendelezo wa promosheni ya Tuzo milionea iliyoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa mwaka jana.

“Kama mtakumbuka mshindi wa droo kubwa ya mwaka jana alikuwa ni Renatus Mkinga, Mkazi wa Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam, ambaye alishinda shilingi milioni 100 na kuboresha maisha yake”.

Akitoa wito kwa wateja wengine kushiriki mara nyingi katika promosheni mbalimbali zinazochezeshwa na kampuni hiyo kwa siku za usoni Bw Correia aliwahakikishia kuwa zitawawezesha kuibuka kidedea na kuboresha maisha yao.

“Tutaendelea kuwekeza ili kuboresha huduma zetu mbalimbali kwa kuwa tunaamini kwamba huduma bora na za uhakika za mawasiliano ni sehemu ya maendeleo, kwani maendeleo ya nchi yoyote yanachangiwa na huduma za mawasiliano zenye uhakika” Alisema.

source nifahamishe