Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia

Monday, May 17, 2010 / Posted by ishak /


Mrembo toka Michigan, Rima Fakih ameshinda mashindano ya urembo wa Marekani Miss USA 2010 na kuwa mwarabu wa kwanza kushinda mashindano hayo makubwa ya urembo nchini Marekani.
Rima Fakih Mmarekani mwenye asili ya Lebanon amekuwa Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kushinda mashindano ya Miss USA katika historia ya mashindano hayo.

Katika mashindano yaliyofanyika mjini Las Vegas na kuonyeshwa live na televisheni ya NBC, Fakih aliwafunika jumla ya warembo 50 toka majimbo mbalimbali ya Marekani na kutwaa taji la Miss USA 2010.

Fakih mwenye umri wa miaka 24, alitwaa taji la urembo wa Marekani akifuatiwa na Miss Oklahoma aliyeshika nafasi ya pili, Miss Virginia, Miss Colorado na Miss Maine.

Fakih ataiwakilisha Marekani kwenye mashindano ya urembo ya Miss Universe yatakayofanyika baadae mwaka huu.


source nifahamishe