Mwanaume na Mwanamke Wabakwa Afrika Kusini

Sunday, May 16, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa mjini Cape Town nchini Afrika Kusini amepandishwa kizimbani kwa kuwabaka wafanyakazi wenzake wawili, mmoja ni mwanaume na mwingine ni mwanamke.
Mwanaume aliyebakwa aliiambia mahakama ya Cape Town kuwa siku ya tukio ambayo kulikuwa na party ya wafanyakazi, alikunywa sana pombe kiasi cha kupitiwa na usingizi.

Mwanaume huyo alisema kuwa alipoamka aliona mambo hayako sawa kwenye maungo yake ya nyuma akihisi hali tofauti.

Mwanaume huyo aliendelea kusema kuwa aligundua kuwa alikuwa amelawitiwa baada ya kurudi kazini siku chache baadae na kusikia wafanyakazi wenzake wakijadili jinsi alivyofanyiwa mchezo mbaya na mwanaume mwenzake.

Mwanaume huyo aliiambia mahakama kuwa aliambiwa na mfanyakazi mwenzake aliyeshuhudia tukio hilo kuwa alimuona mfanyakazi mwenzao akijiandaa kumbaka lakini hakuchukua hatua yoyote.

Mwanaume huyo aliongeza kuwa alienda polisi ambapo alifanyiwa uchunguzi uliothibitisha kuwa aliingiliwa kinyume cha maumbile.

Mwanamke aliyebakwa ni mpenzi wa shuhuda aliyemuona mwanaume akibakwa.

Mwanamke huyo alisema kuwa mtuhumiwa alimkaba koo kwa nguvu na alipozimia mtuhumiwa alimbaka na kumuibia simu yake.

Ripoti ya daktari ilithibitisha kuwa mwanamke huyo alibakwa.

Mtuhumiwa amekanusha madai yote mawili ya ubakaji. Uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment