Aua Watu Wawili Ili Ahukumiwe Kunyongwa

Thursday, December 17, 2009 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini China ambaye alikuwa na nia ya kujiua baada ya kushindwa kupata kazi kwa muda mrefu, amewaua watu wawili ili ahukumiwe kunyongwa.
Mwanaume huyo alikuwa na nia ya kujiua lakini alikuwa hana ujasiri wa kuitoa roho yake mwenyewe. Aliamua kuwaua watu wawili ili ahukumiwe adhabu ya kunyongwa.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alitajwa kwa jina moja tu la Bin, alichukua uamuzi huo kutokana na hali ngumu ya maisha aliyokuwa nayo baada ya kushindwa kupata kazi kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya mji wa Jiangmen katika jimbo la Guangdong, Bin aliwaua watu wawili kwa kuwanyonga ili ahukumiwe adhabu ya kifo.

"Kwa muda mrefu sina kazi, sina uwezo wa kujiua mwenyewe, nimefanya mauaji ili nihukumiwe kunyongwa", alisema Bin.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi, Bin hana uhusiano wowote na wala alikuwa hawajui watu aliowaua.

source.nifahmishe.com

0 comments:

Post a Comment