MWanamke afia gesti kuitatanishi, Kimara

Thursday, December 17, 2009 / Posted by ishak /

MWANAMKE ambaye hakuweza kufahamika jina wala makazi yake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30, amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Marangu huko Kimara jijini Dar es salaam.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 5 asubuhi, huko maeneo ya Kimara Mwisho.


Alisema maiti ya mwnwamke huyo ilikutwa ikiwa imelala kitandani huku mdomoni ikiwa inatoka mapovu na haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha kifo hicho.


Alisema kuwa, mwanamke huyo alifika katika gesti hiyo Desemba 13, majira ya saa 4 asubuhi na alipanga katika nyumba hiyo akiwa na kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James Joshua, mkazi wa jijini Dar es Salaam.


Katika maelezo yaliyopatikana katika nyumba hiyo ilidaiwa kuwa, kwa mara ya mwisho mwanamume aliyeuingia gesti na dada huyo aliaga kwa mhudumu mmoja alyekuwa zamukuwa anakwenda kutafuta chakula aina ya chipsi na hakurejea tena.


Amesema baada ya wahudumu kutaka kuingia katika chumba hicho kwa nia ya kufanya usafi, ndipo walipobaini dada huyo kuwa aklikuwa ameshakufa.

Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea kumsaka kijana huyo kwa udi na uvumba.


source.nifahmishe.com

0 comments:

Post a Comment