Mwanamke Ajifungua Mtoto Gym Akinyanyua Vyuma

Thursday, December 17, 2009 / Posted by ishak /


Mwanamke aliyeiwakilisha nchi ya Chile kwenye mashindano ya Olimpiki ya kunyanyua vitu vizito, alikuwa hajui kama ana mimba, amejifungua mtoto ndani ya gym wakati akifanya mazoezi ya kunyanyua vyuma.
Elizabeth Poblete, 22, mwanamichezo aliyeiwakilisha Chile kwenye mashindano ya kunyanyua vitu vizito kwenye olimpiki mwaka jana nchini China, amejifungua mtoto ndani ya gym alipokuwa akifanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito.

Elizabeth alikuwa hajui kama ana mimba na alijifungua mtoto huyo kwenye gym iliyopo kwenye mji wa Sao Paulo nchini Brazili alikoweka makazi yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na tovuti ya habari ya Globo.com, Elizabeth alijifungua mtoto wa kiume ambaye amempa jina la Eric Jose.

Akiongelea tukio hilo kocha wake wa gym, Horacio Reis, alisema kuwa alikuwa hajui kama Elizabeth alikuwa na mimba kwani wiki iliyopita aliweza kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya kubeba vyuma yaliyofanyika nchini Chile.

"Mashindano yalimalizika salama na alishinda", alisema kocha wake.

Kwa mahesabu ya madaktari, Elizabeth alikuwa na mimba ya miezi sita lakini kutokana na lishe na mazoezi aliyokuwa akifanya, mzunguko wake wa damu za hedhi ulikuwa hauna mpangilio maalumu hivyo kumfanya asigundue kuwa ana mimba.

Elizabeth aliiwakilisha Chile kwenye mashindano ya olimpiki yaliyofanyika Beijing, China mwaka jana.

Katika miezi ya karibuni, alikuwa kwenye mazoezi makali na lishe ya nguvu ili kuupandisha uzito wake kutoka kilo 75 hadi 85.


source.nifahamishe.
com

0 comments:

Post a Comment