Mtoto wa Miaka 10 Apandishwa Kizimbani Kwa Ubakaji

Thursday, December 17, 2009 / Posted by ishak /


Watoto wawili wa kiume wa nchini Uingereza wenye umri wa miaka 10 wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8.
Watoto hao wakisindikizwa na ndugu zao walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Uxbridge, magharibi mwa mji wa London, wakikabiliwa na kesi ya ubakaji.

Katika tukio hilo lililotokea oktoba 27 mwaka huu, watoto hao wanatuhumiwa kushirikiana kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane wakati walipokuwa wakicheza kwenye bustani ya Hayes, iliyopo magharibi mwa London.

Watoto hao kila mmoja amefunguliwa mashtaka mawili ya ubakaji.

Waliachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi wa kesi yao ukiendelea na watapandishwa tena kizimbani tarehe 28 mwezi ujao.

Kutokana na umri wa watuhumiwa hao, vyombo vya habari vimewekewa masharti na mahakama katika kuripoti tukio hilo.

Vyanzo vya mahakama vimeelezea kushtushwa na kesi hii ya ubakaji kutokana na umri mdogo sana wa watuhumiwa.

Kwa mujibu wa sheria za Uingereza umri wa mtoto kufunguliwa mashtaka ya jinai ni miaka 10. Nchini Scotland sheria zinaruhusu kuwafunguliwa mashtaka watoto wenye umri wa miaka minane. Umri huo ndio mdogo kulinganisha na nchi zingine za barani ulaya.

source.nifahmishe.com

0 comments:

Post a Comment