Mwanaume mmoja nchini Uingereza amejikuta akipandishwa kizimbani kwa kosa la kumuua mpenzi wake wakati wakifanya mapenzi.
Vionjo katika malavidavi havikumuendea vizuri bwana Jason O'Malley, 39, ambaye amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua mpenzi wake.
Jason ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake watatu tofauti kwa wakati mmoja, aliiambia mahakama kuwa mpenzi wake Kerry Sneddon alikuwa akimtaka awe anaikandamiza shingo yake kwa nguvu wakati wa kupeana uroda.
Jason aliwaambia maafisa wa polisi alipotiwa mbaroni kuwa ingawa alikuwa hapendi, alifuata maagizo ya mpenzi wake ya kumkaba koo kwa nguvu wakati wa kufanya mapenzi.
Jason aliongeza kuwa walishawahi kufanya hivyo mara sita au saba kabla ya siku ya tukio la kufariki kwa mpenzi wake.
Mwili wa bi Sneddon ulikutwa ukiwa hauna nguo kwenye sakafu. Shingo yake ilionyesha kuwa alikabwa koo kwa kutumia waya.
Jason aliwaambia polisi kuwa anakumbuka jinsi walivyoanza kufanya mapenzi lakini hakumbuki kitu kilichopelekea kufariki kwa mpenzi wake. Jason aliongeza kuwa hawakuwahi kutumia waya kabla ya siku hiyo.
Jason alikanusha kumuua mpenzi wake huyo ambaye alifahamiana naye kupitia mitandao ya internet ya kutafuta wachumba. Hata hivyo upande wa mashtaka umeukataa utetezi wa Jason ukisema kuwa Jason alimuua mpenzi wake baada ya kutokea marumbano kati yao.
"Mtuhumiwa alimuua Kerry Sneddon, hatukubali kuwa hii ni ajali, alitumia waya kumkaba koo na alitumia nguvu nyingi sana akiwa na nia ya kumuua au kumdhuru", mwendesha mashtaka aliiambia mahakama.
Mahakama iliambiwa kuwa Jason alikuwa na wivu sana akichungulia kila meseji iliyokuwa ikiingia kwenye simu ya bi Sneddon na pia akitaka kujua kila sehemu anayoenda.
Jason alianza kuishi na bi Sneddon mwaka 2007 baada ya kumtelekeza mkewe.
Uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment