WAKAZI wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamekuwa wakikesha wilayani humo usiku na mchana wakisubiria pesa zinazotoka chini ya mti mithili ya chemchem.
Baadhi ya Wakazi wa mji huo inasemekana waligundua maajabu hayo kwenye mti huo na baada ya wakazi hao kuanza kujizolea pesa toka kwenye mti huo habari ghafla zilisambaa mkoani Ruvuma kuwa kuna mti una chemchem ya pesa.
Ilidaiwa kuwa wakazi hao walipokuwa wakipita chini ya mti huo waliona pesa zikitoka chini ya mti na pamoja na kustaajabishwa na tukio hilo wakazi hao waliamua kuzichukua pesa hizo.
Taarifa zaidi zilisema kwamba kwa muda wa siku mbili mfulululizo wakazi wa wilaya ya Songea waliendelea kuziokota pesa zilizokuwa zikitoka kwenye mti huo.
Pesa hizo inadaiwa zilikuwa zikitoka mithili ya chemchem zikiwa ni noti tofauti tofauti zikiwemo na noti za shilingi elfu kumi, tano na kadhalika.
Baadhi ya watoto waliowahi kuhojiwa na mwakilishi wetu wa nifahamishe kutoka eneo la tukio, watoto hao walidai kuwa walishajizolea pesa hizo na walizipeleka kwa wazazi wao nyumbani.
Walidai kuwa pesa hizo zilikuwa zikitoka chini ya ardhi na mamia ya watu toka sehemu mbalimbali za mkoani Ruvuma walikuwa wakizigombania kila zilipoanza kuchomoza.
Watu wazima waliohojiwa na Nifahamishe nao pia walithibitisha kujizolea noti hizo zilizodaiwa kutoka kwenye chemchem hiyo.
Kwa kuwa pesa pesa hizo zilikuwa zinatumia muda mrefu kutoka kwenye chemchem hiyo, maelfu ya watu kutoka wilaya tofauti wamekuwa wakiweka kambi eneo hilo kusubiria pesa hizo.
Tukio hilo limethibitishwa na polisi mkoani humo na walisema wanafanya uchunguzi wa kina kubaini kuwa pesa hizo zinakuwa zinatoka wapi.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment