Bingwa wa Zamani wa Ndondi Ajinyonga

Monday, April 19, 2010 / Posted by ishak /


Bingwa wa zamani wa dunia wa ndondi za uzito mwepesi za mashirikisho ya ndondi ya WBC na WBA, Edwin Valero amejinyonga kwa kutumia nguo zake ikiwa ni masaa 48 baada ya kutupwa mahabusu kwa tuhuma za kumuua mke wake.
Edwin Valero, raia wa Venezuela ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa mashirikisho ya WBA na WBA katika uzito mwepesi, amejinyonga mwenyewe kwa kutumia nguo zake ndani ya selo ya polisi alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchomachoma na kisu.

Polisi walimtia mbaroni Valero siku ya jumapili baada ya kuukuta mwili wa mkewe Jennifer, 24, kwenye chumba cha hoteli moja mjini Valencia, Venezuela.

Valero alikuwa akitambulika kama shujaa wa Venezuela kutokana na rekodi yake nzuri kwenye ndondi. Alishinda mapambano yake yote 27 ya kimataifa kwa knockout.

Taarifa zinasema kuwa Valero mwenye umri wa miaka 28, aliondoka hotelini hapo majira ya alfajiri ya siku ya jumapili akiwaambia walinzi wa hoteli kuwa amemuua mke wake aliyezaa naye watoto wawili.

Valero inaripotiwa kuwa alikuwa na makosa kadhaa ya uvunjaji wa sheria. Alipigwa marufuku kuendesha gari nchini Marekani na mwezi uliopita alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe na kisha kuwatishia maisha madaktari waliokuwa wakimpatia tiba mkewe.


source nifahamishe