Amzalisha Binti Yake Watoto 7

Friday, June 11, 2010 / Posted by ishak /Mvuvi wa nchini Brazili ambaye alikuwa akimbaka mtoto wake kwa miaka 16 na kupelekea kuzaa naye watoto 7 ametiwa mbaroni.
Mvuvi toka maeneo ya watu masikini ya Maranhao nchini Brazili ambaye alikuwa akimwingilia kinguvu binti yake kwa miaka 16 ametiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Brazili la Estado, polisi walimtia mbaroni Jose Agostinho Bispo Perreira mwenye umri wa miaka 54 baada ya kupewa taarifa na mtu asiyejulikana juu ya mchezo wa mzee huo kula mayai yake mwenyewe.

Taarifa zinasema kuwa Perreira alianza mchezo wa kumuingilia binti yake tangia alipokuwa na umri wa miaka 12.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Perreira alimfungia binti yake huyo kwenye kibanda kilichopo mbali na mji aliokuwa akiishi.

Polisi waliokuwa wakimfanyia uchunguzi Perreira wamegundua kuwa hivi sasa binti yake ana umri wa miaka 28, hajui kusoma wala kuandika na amezaa watoto saba na Perreira.

Mtoto mdogo kuliko wote ana umri wa miezi miwili wakati waliobakia wana umri wa miaka 4, 5, 7, 8 na 12.

Polisi wanasema kuwa Perreira alikuwa akiwagawa kwa familia zingine watoto aliozaa na binti.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa mvuvi Perreira alianza kuishi na binti yake baada ya ndoa yake na mkewe kuvunjika.

Perreira alizaa watoto wanne na mkewe huyo. Watoto wake wawili wa kiume na mmoja wa kike walienda kuishi na mama yao mji mwingine.

Hawakuwa na taarifa kuwa baba yao alikuwa akimuingilia kwa nguvu mdogo wao na alizaa naye watoto saba.

source nifahamishe