Baada ya Ajali Mtoto wa Miaka 3 Awa Chapombe na Mvutaji Sigara

Thursday, June 10, 2010 / Posted by ishak /Baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya gari, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu nchini China amekuwa mvutaji sigara na mlevi.
Baada ya kugongwa na gari mwaka jana, mtoto Ya Wen wa nchini China amegeuka kuwa mvutaji sigara sugu na mlevi.

Ajali hiyo imebadilisha kabisa maisha ya Wen kwani siku hizi anapenda kuvaa nguo za kiume na hulia sana wazazi wake wanapokataa kumnunulia nguo za kiume anazozitaka.

Wazazi wake ambao hufanya kazi ya kukusanya taka na kuziuza ili kupata pesa za kujikimu, siku hizi wanalazimika kuzibana bajeti zao ili waweze kumnunulia ulabu na sigara binti yao.

Wen aligongwa na lori mwaka jana, aliwahishwa hospitali ambako alilazwa wiki moja akipatiwa matibabu. Aliruhusiwa kurudi nyumbani lakini alitumia miezi kadhaa kurudia hali yake ya zamani.

Wiki moja baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani toka hospitali, Wen alikutwa na mama yake akiwa amejificha anavuta sigara.

Haukupita muda Wen alianza kuiba sigara za baba yake na pia toka kwenye maduka madogo madogo ya jirani.

Mama yake Wen aliyetajwa kwa jina la Gao, alisema kuwa binti yake amekuwa mvutaji sigara aliyekubuhu na pia amekuwa mlevi.

"Chupa tatu za bia sio tatizo kwake", alisema mama huyo.


source nifahamishe