Mwalimu Arekodi Video Akimlawiti Mwanafunzi Wake

Monday, June 07, 2010 / Posted by ishak /


Sunday, June 06, 2010 1:53 AM
Mwalimu mmoja wa kiume wa nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka 17 baada ya kurekodi video akimlawiti mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 15.
Aliyekuwa mwalimu wa wa shule msingi ya Cedar Lee Middle School ya Virginia, Marekani, Scott Christopher Howe amehukumiwa kwenda jela miaka 17.5 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume na pia kurekodi video akifanya kitendo hicho.

Scott mwenye umri wa miaka 34 alirekodi jumla ya video 22 akimlawiti mwanafunzi wake ambaye alikuwa na umri wa miaka 15.

Baadhi ya video hizo zilirekodiwa ndani ya mabafu na madarasa ya shuleni kwake.

Video 9 zilipatikana kwenye laptop ya Scott wakati video zingine 13 zilipatikana kwenye external hard drive.

Polisi walimkamata Scott baada ya kuitwa nyumbani kwake na mwenye nyumba wake ambaye alidai Scott analima bangi ndani ya nyumba yake.

Wakati polisi wakisaka mimea ya bangi ndani ya nyumba yake, waligundua kompyuta yenye kamera iliyoelekezwa kitandani. Walipodadisi vilivyomo kwenye kompyuta hiyo ndipo walipokutana na video za Scott akimlawiti mwanafunzi wake.

Mwanafunzi huyo aliwaambia polisi kuwa alikuwa akifahamu kwamba Scott hurekodi video anapomuingilia kinyume cha maumbile.

Polisi pia waligundua mimea 15 ya bangi ndani ya chumba cha Scott.

Akisomewa hukumu yake jana Scott alihukumiwa kwenda jela miaka 17.5 ingawa upande wa mashtaka ulitaka mahakama itoe adhabu kubwa zaidi.

source nifahamishe