Hauwezi Kuolewa Kwasababu Huna Akili, Hujui Maana ya Ndoa

Monday, September 14, 2009 / Posted by ishak /


Yalikuwa yamebaki masaa 48 kabla ya harusi kufungwa na sherehe kubwa za harusi kuanza, wakati bibi harusi ambaye alikuwa tayari ni mjamzito alipoambiwa kuwa wewe huwezi kuolewa kwasababu huna akili hujui nini maana ya ndoa.
Kerry Robertson, ambaye ana kichwa kigumu kuelewa, mkazi wa Fife, Scotland aliambiwa kuwa harusi yake imefutwa masaa 48 kabla ya kuvaa shela lake la harusi kufunga ndoa na mchumba wake Mark McDougall.

Kerry mwenye umri wa miaka 17 alikuwa ameishanunua gauni lake la harusi, yeye na mchumba wake walikuwa wameishanunua pete za harusi na sherehe kubwa baada ya kufungishwa ndoa kanisani ilikuwa imeandaliwa kufanyika jumamosi iliyopita.

Lakini siku mbili kabla ya harusi, maafisa wa ustawi wa jamii walimwambia bibi harusi kuwa harusi yao imefutwa kwasababu "haelewi chochote kuhusiana na maisha ya ndoa".

Kerry ambaye ana ujauzito wa miezi mitano alitoa malalamiko yake jana akisema kuwa uamuzi uliotolewa wa kuifutilia mbali harusi yake ni wa kikatili.

"Bado nina huzuni sana, najua ndoa nini. Ni wapenzi wawili kuamua kutumia maisha yao yote wakiishi pamoja. Nampenda Mark na nataka kuwa mke wake" alisema Kerry.

Kerry alikuwa akilelewa na bibi yake tangia alipokuwa na umri wa miaka 9 baada ya wazazi wake kushindwa kumtunza vyema, na gharama zote za matunzo yake zilikuwa zikitolewa na ofisi ya ustawi wa jamii.

Mwezi januari mwaka huu, Kerry alikutana na McDougall mwenye umri wa miaka 25 na kuanza uhusiano wa kimapenzi. Kerry alipopata mimba waliamua kufunga ndoa.

McDougall alisema kuwa balaa hilo lilianza alhamisi iliyopita wakati maafisa wawili wa ustawi wa jamii walipofika kwenye nyumba yao waliyokuwa wakiishi pamoja na kuwaambia kuwa ndoa yao ni kinyume cha sheria kwakuwa Kerry ana upungufu wa akili na hana uwezo wa kujiamulia mambo mwenyewe.

"Kerry aliangua kilio hapo hapo". "Pamoja na kujibishana nao sana tukiwaambia kuwa tunapendana na tusingependa mtoto wetu azaliwe wazazi wake tukiwa hatujaoana, hawakutaka kutuelewa na walishikilia uamuzi wao huo", alisema McDougall.

Kwa mujibu wa sheria za Scotland, afisa wa serikali anayefungisha ndoa, anaweza kuivunja harusi kama ataona kuwa mmoja wa maharusi au wote wawili wana upungufu wa akili na hawajui chochote kuhusiana na ndoa.

source.nifahamishe.com

0 comments:

Post a Comment