Mtoto Mapacha Azaliwa bila Kichwa Afghanistan

Monday, September 14, 2009 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja wa nchini Afghanistan amejifungua watoto wawili mapacha walioungana kwenye kifua huku pacha mmoja akiwa hana kichwa.
Mwanamama mmoja wa nchini Afghanistan amejifungua watoto wawili mapacha wa kiume walioungana kwenye sehemu za kifua pekee huku pacha mmoja wapo akiwa hana kichwa.

Pacha ambaye hana kichwa alizaliwa akiwa amekamilika viungo vyote vingine vya binadamu kasoro kichwa tu.

Alikuwa na kiwiliwili cha juu, mikono, miguu na viungo vingine isipokuwa kichwa pekee ndicho kilichokosekana.

Mapacha hao walizaliwa siku ya alhamisi katika hospitali moja kaskazini mwa Afghanistan.

"Kwa siku chache za mwanzo pacha ambaye hakuwa na kichwa alikuwa hai na alikuwa akiisogeza sogeza mikono na miguu yake, lakini hivi sasa amefariki" alisema Dr Homayoun Khamoosh wa hospitali ya mji wa Kunduz walikozaliwa mapacha hao.

"Hii ni mara ya kwanza tunaona mapacha kama hawa kwenye mji huu wa Kunduz" alisema Dr Homayoun.

Dr Khamoosh alisema kuwa mapacha hao wanahitaji kufanyiwa operesheni ya kuwatenganisha haraka iwezekanvyo ili kuokoa maisha ya pacha aliyezaliwa akiwa amekamilika viungo vyote.

"Madaktari wameamua kufanya operesheni ya kuwatenganisha mapema kabla ya mwili wa pacha ambaye hana kichwa aliyefariki haujaanza kuharibika", alidokeza Dr Khamoosh.

Mama wa mapacha hao mwenye umri wa miaka 35 ambaye ana watoto wengine wanne, alijaribu kuficha sura yake kwa waandishi wa habari na alikataa kutaja jina lake.



source.nifahamishe.com

0 comments:

Post a Comment