17 wa ukoo mmoja wauawa kinyama Mara

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak /

WATU 17 wa ukoo mmoja kutoka familia tatu wameuawa kikatili kwa kwa kuchinjwa kama kuku kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana katika mtaa wa Bhugharanjabho Kata ya Buhare huko mkoani Mara.
Mbali na kuwanjinjaw atu hao pia waharifu hao walifanya uharibifu kuuwa mifugo ya marehemu hao walikatakata ng’ombe na mbuzi na kuacha mizoga katika mji huo.

Tukio hilo la kihistoria na la kutisha na la kwanza kutokea mkoani Mara, lilitokea usiku wa kuamikia jana, majira ya saa 8 usiku katika kata hiyo.

Familia ya kwanza iliyochinjwa katika tukio hilo ni ile ya Kawawa Kinguye ambapo mke na watoto wake watano waliuawa, familia ya pili ni ile ya mdogo wake Kinguye aitwae Moris Mgaya iliweza kupoteza watu sita, familia ya tatu ni ile ya binamu yao aliyetambulika kwa jina la Mgaya Nyarukende pia watu watano waliuawa katika familia hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Enos Mfuru.aliliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kufunga ofisi zao mara moja na kuanza msako mkali na kwa gharama yoyote dhidi ya watu waliofanya mauaji hayo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo.

Na kuwataka wananchi waishio maeneo hayo kutoa ushirikiano wa kutosha kuwasaka wauaji hao ambao utafanikisha kutiwa mbaroni watuhumiwa hao haraka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, alisema tayari kikosi kikubwa cha askari wake kisambazwa kila kona kuanza msako huo ili kuhakikisha watu wote waliohusika wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Ilidaiwa kuwa tukio hilo linavyosemekana ni la visasi, taarifa ambazo zilipatikana jana katika eneo la tukio zilidai kuwa huenda tukio hilo likahusishwa na ulipishaji kisasi kutokana na marehemu Kawawa kuwahi kutuhumiwa kuua watu wawili waliodhaniwa ni wezi wa mifugo, lakini baadaye ikabainika kuwa walikuwa wameua na nungunungu.

Mwaka 2006 baada ya Kawawa kuachiwa, watu wasiojulikana walivamia boma lake na kuua mama na dada yake Kawawa na kuahidi kuwa wangerudi tena na kuhisiwa huenda tukio hilo ni wale watu walioahidi wangerudi.

Taarifa hizo ziliendela kusema kuwa, marehemu Kawawa aliachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kuonekana hana hatia na kukuta ndugu zake hao walikwisha kuuawa na watu hao na kwamba tangu wakati huo aliendelea kuishi eneo hilo hadi hapo jana nay eye yalipomkuta umauti.

Hadi jana saa 12 jioni polisi walikuwa wakizifanyia uchunguzi maiti hizo katika eneo la tukio kutokana na kuwa katika hali mbaya, kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Geofrey Ngatuni, miili ya watu hao inatarajiwa kuzikwa leo endapo uchunguzi huo utakamilika.

source nifahamishe