Aanguka toka ghorofa ya tisa

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak /

FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Ally, amekufa baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tisa wakasti akiwa katika shughuli za ujenzi katika ghorofa hiyo.

Fundi huyo alikuwa katika ya nyumba ya Shubas Patel iliyokuwa na ghorofa 12 na alianguka wakati akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema ajali hiyo ilitokea jana, saa 10 jioni, Mtaa wa Sewa na Zanaki Ilala jijini Dar es Salaam.

Alisema fundi huyo, akiwa na wenzake wakiendelea na kazi kwenye ghorofa ya tisa, ghafla alidondoka hadi ghorofa ya tatu ambapo alinasa kwenye kizuizi cha mabati.

Alisema alipata majeraha kwenye paji la uso pamoja na kuvunjika mkono wake wa kushoto.

Hata hivyo wenzake walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.


source nifahamishe