Mwanajeshi amcharanga mkewe kwa visu

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak /

MWANAJESHI Mstaafu wa Jeshi la JWTZ, Mang'eng'e Matiko, amemchoma kisu mkewe baada ya kutopatikana kwa maelewano katika ugomvi wa ardhi.

Ilidaiwa kuwa mwanajeshi huyo alimchoma kisu mkewe katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kuanguka ghafla baada ya mwanamke huyo kukataa kuuzwa kwa ardhi waliyokuwa wakiimiliki wote kwa pamoja.

Mume huyo alitaka kuuza ardhi hiyo lakini mwanamke huyo alipinga kuuzwa kwa ardhi hiyo kwa kudai ingewasaidia baadae kwa kuwa walikuwa na watoto.

Hivyo baada ya mabishano hayo mwanajeshi huyo alichukua uamuzi wa kumchoma kisu mkewe na kupelekea majeruhi hayo.


Majirani wa familia hiyo walidai kuwa alichukua uamuzi wa kumchoma visu katika sehemu za mwili wake na aliweza kuokolewa baada ya mwanamke huyo kupiga kelele na majirani kufika nyumbani kwao hapo na kumkuta wmanamke huyo anatoka damu nyingi na ghafla alipoteza fahamu.


Walidai kuwa mwanamke huyo hali yake ilikuwa mbaya na alipelekwa katika kituo cha Polisi Karakata baaada ya polisi kufika eneo hilo na kutumia gari la polisi lililokuwa na namba T 481 AER aina ya Land Rover Defender na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

source nifahamishe