Picha ya Yesu Akinywa Pombe Yazua Kasheshe India

Saturday, February 20, 2010 / Posted by ishak /


Serikali ya India imelazimika kuvikusanya vitabu vyote vya shule za msingi vilivyochapishwa na kampuni moja nchini humo vikiwa na picha ya Yesu akinywa pombe huku akiwa ameshikilia sigara.
Serikali ya India katika jimbo la Meghalaya inavikusanya vitabu vipya vilivyochapishwa kwaajili ya shule za msingi nchini humo vikiwa na picha ya Yesu akiwa ameshikilia kopo la bia mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa ameshikilia sigara.

Vitabu hivyo vilianza kutumika kwenye shule za msingi na picha hiyo ya Yesu imesababisha kasheshe kubwa katika jimbo hilo la Meghalaya ambalo asilimia 70 ya wakazi wake ni wakristo.

Waziri wa elimu wa jimbo hilo Ampareen Lyngdoh amesema kuwa taratibu za kisheria zimeanza kuandaliwa dhidi ya kampuni iliyochapisha vitabu hivyo.

"Tunajiandaa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Skyline Publications ambayo imechapisha vitabu vilivyozua mtafaruku," alisema waziri Mr Lyngdoh.

Picha hiyo ya Yesu ilikuwa kwenye kava la vitabu vya mazoezi ya kuandika kwa shule za msingi.

Waziri Lyngdoh amesema kuwa vitabu hivyo vilianza kutumika kwenye shule za msingi za binafsi na serikali ya India imeamua kuvikusanya vitabu vyote vyenye picha hiyo toka kwenye mashule yote ya India na kwenye maduka ya vitabu.

Kampuni ya Skyline Publications yenye makazi yake mjini New Delhi haijasema chochote kuhusiana na tukio hilo.

source nifahamishe

1 comments:

Anonymous on November 24, 2010 at 9:06 AM

Nikweli selikali ifanye juu chini kuchukua hatua za kinidhamu ili kuiadhibisha kampuni hiyo ambayo ime buni mambo hayo ambayo hayajawahi kutokea Duniani.Nimesoma vitabu vyote tangu kuzaliwa kwa yesu hadi kufa kwake na utumishi wake aliokuwa nao Duniani sijawahi kukutanana msitari unao zungumzia kwamba yesu aliwahi kunywa pombe wala kuvuta sigara hivyo hili litiliwe mkazo zaidi kabla mambo haya jawa magumu"

Post a Comment