Mwanamke Atupwa Jela Miaka 25 Kwa Kumuua Mbakaji Wake

Tuesday, February 16, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda jela miaka 25 kwa moyo wa ukatili aliouonyesha wa kumuua mbakaji wake na kisha kuifukia maiti yake kabla ya kuifukua na kuwalisha mamba maiti hiyo.
Michelle Nadasen mama wa mtoto mmoja wa nchini Afrika Kusini ametupwa jela miaka 25 kwa kumuua mbakaji wake na kisha kuwalisha mamba maiti yake.

Michelle mwenye umri wa miaka 23 alimuua mwanaume aliyemnyanyasa kijinsia na kisha kuizika maiti yake mbele ya nyumba yake.

Siku ya nne baada ya kuizika maiti hiyo, Michelle kwa kushirikiana na mpenzi wake waliifukua maiti hiyo na kuitupa kwenye mto wenye mamba wengi.

Akisomewa hukumu katika mahakama kuu ya mji wa Pietermaritzburg, jaji wa kesi hiyo alisema kuwa Michelle ameonyesha moyo wa kikatili na usio na utu kwa kulala siku nne katika nyumba ambayo maiti ya mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Gansen Gounden ilikuwa imefukiwa.

Michelle alikiri kosa lake na kuelezea jinsi yeye na mpenzi wake walivyoizika maiti ya Gounden katika shimo la futi chache walilochimba chini ya mwembe uliopo nyuma ya nyumba yao.

Michelle pia aliielezea mahakama jinsi alivyosaidiana na mpenzi wake kuitupa maiti ya Gounden kwenye mto Enseleni wenye mamba wengi.

source nifahamishe