Amuua Mkewe Kwa Kuchati Online na Mwanaume

Sunday, April 11, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja nchini Jordan anashikiliwa na polisi baada ya kumuua mkewe miezi sita baaa ya ndoa yao akidai kuwa alimfumania akichat online na mwanaume mwingine.
Mtuhumiwa alimkaba koo mkewe mwenye umri wa miaka 37 kabla ya kukipasua kwa nyundo kichwa chake na kisha kujaribu kuutupa mwili wake”, alisema msemaji wa polisi.

“Alijaribu kuuchoma moto mwili wake lakini alishindwa. Alidai kuwa mkewe alikuwa na tabia mbaya ya kuchat na mwanaume kwenye internet”, aliendelea kusema msemaji huyo wa polisi.

Mtuhumiwa huyo ambaye ana umri wa miaka 30 anashikiliwa na polisi na anakabiliwa na adhabu ya kifo.

”Baada ya mauaji alitoa taarifa kwa wakwe zake kuwa mkewe amepotea na hajui alipo wakati huo huo watu wengine wawili walienda kutoa taarifa polisi”, alisema msemaji wa polisi.

Lakini hata hivyo kutokana na taarifa zake za utatanishi polisi walimhisi yeye ndiye aliyefanya mauaji ya mkewe.

Baada ya kubanwa sana na polisi mwanaume huyo aliamua kukiri kumuua mkewe akisema kuwa alikuwa hapendi tabia ya mkewe kuchat na mwanaume kwenye internet.

source nifahamishe