Ukimfumania Mumeo na Kondomu Mpongeze'

Wednesday, April 14, 2010 / Posted by ishak /


Mkufunzi mmoja ambaye ni nguli wa kuwafunda akina dada wakati wa Kitchen Party amewataka akina dada ambao wanakwenda kuolewa kufahamu vizuri jinsi ya kuutumia mwiko wa kupikia kwenye chungu ili kuzidumisha ndoa zao na pia wasiwe na ghadhabu wanapokuta kondomu kwenye mifuko ya suruali ya waume zao.
Nguli huyo maarufu jijini Dar es Salaa kwa masuala ya Kitchen Party [Jina Kapuni] alikuwa akitoa mafunzo katika sherehe mojawapo iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, hivi karibuni.

"Katika ndoa kuna mengi yanayojitokeza mbali na kufanya kazi za nyumbani, unaweza kukuta katika suruali ya mume wako ndani ya mfuko amesahau Kondomu ukiona hivyo mpongeze mume wako maana anakujali pia usichukie wewe iweke vizuri na ikiwezekana pindi anaposafiri nenda dukani kamwongezee boksi nyingine ,mfungie kwenye begi lake", alisema kungwi huyo.

Kungwi huyo alimwambia pia bibi harusi kuwa ukiona mwanamke mwenzako jirani yako amekuja kwako kukwambia kwamba mume wako ana uhusiano na mwanamke mwingine basi mchukulie mwanamke huyo kuwa anataka kuharibu ndoa yako.

Mambo yako ya ndani usimwambie mtu mwingine zaidi ya mume wako maana ukisema mume wako anakojoa kitandani atakayechekwa ni wewe mwenyewe", alimalizia kusema mama huyo.

Alisema pia kuwa wengi wa wasichana wanapoolewa huwa hawajui maana ya huu mwiko ambao alikuwa ameushikilia akimwelezea bibi harusi mtarajiwa jina tunalihifadhi.

Alisema utakuta akina mama watu wazima ambao tayari wameolewa wanakuwa wanachanganya mwiko katika vyungu mbalimbali jambo ambalo halitakiwi mwiko unatakiwa kuingia katika chungu kimoja tu ni cha mme wako ambaye amekuoa na si vinginevyo.

"Mwiko ukitumika katika vyungu vingi hupoteza ladha" alisema nguli huyo.

Alifafanua kuwa wengi wa akina mama walioolewa wamekuwa wakithubutu kwenda nje ya ndoa zoa na hivyo miili yao kuingiliwa na miiko zaidi ya mmoja ambapo hasara yake ni kuambukizwa magonjwa.

source nifahamishe