Azinduka Toka Kwenye Koma na Kuanza Kuzungumza Kijerumani

Wednesday, April 14, 2010 / Posted by ishak /


Msichana mmoja wa nchini Croatia amewashangaza watu wengi baada ya kuzinduka toka kwenye koma baada ya kupoteza fahamu kwa masaa kadhaa akiwa ameisahau kabisa lugha yake halisi na kuanza kubonga kijerumani kama vile alizaliwa nacho.
Msichana huyo ambaye alipoteza fahamu kwa masaa 24 wiki mbili zilizopita, amewaacha madaktari wakiumiza vichwa kutokana na hali aliyo nayo.

Msichana huyo alizinduka akiwa ameisahau kabisa lugha yake ya Croatia na kuanza kuzungumza kijerumani fasaha kama vile alizaliwa nacho.

Wazazi wake walisema kuwa msichana huyo alikuwa akijifunza kijerumani shuleni na pia akiangalia shoo za kijerumani kwenye luninga lakini kijerumani kilikuwa hakipandi kabisa akishindwa hata kuziunga sentesi kifasaha.

"Huwezi kujua ukizinduka toka kwenye koma ubongo utakuwa katika hali gani", alinukuliwa mkurugenzi wa hospitali ya KB Hospital ambayo msichana huyo alikuwa amelazwa.

Madaktari kadhaa wamejaribu kumfanyia uchunguzi msichana huyo lakini wameshindwa kujua chanzo cha hali iliyomtokea.

source nifahamishe