Mama Amuua Mtoto Wake na Kuliuza Sikio Lake Kwa Mganga

Tuesday, July 06, 2010 / Posted by ishak /


Mama mmoja nchini Zimbabwe amemuua mtoto wake wa miezi 18 na kisha kulikata sikio lake moja na kumuuzia sikio hilo mganga wa nchini Msumbuji kwa dola 20.
Christine Hofisi mwenye umri wa miaka 21 anayeishi katika kitongoji cha Chipinge nchini Zimbabwe karibu na mpaka wa nchini Msumbiji, alimuua mtoto wake mchanga wa kiume mwenye umri wa miaka 18 na kisha kulikata sikio lake la kushoto na kumuuzia mganga anayeishi nchini Msumbiji.

Mwili wa mtoto huyo aliyepewa jina la Edmore uligunduliwa na majirani kwenye kichaka kilichopo karibu na nyumba ya mwanamke huyo.

Christine aliliuza sikio la mtoto wake kwa dola 20 kwa mganga anayeishi karibu na mpaka nchini Msumbiji anayeitwa Maheza.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Christine alipewa dola 10 na dola 10 zilizobaki aliahidiwa kulipwa baadae.

Mganga Maheza anatafutwa na polisi akituhumiwa kwa mauji ya watu wengine kadhaa baada ya mafuvu 11 ya binadamu kukutwa ndani ya nyumba yake.

Polisi nchini Zimbabwe wamesema kuwa wanamhoji Christine kwa mauaji ya mtoto wake na wataenda nchini Msumbiji kushirikikiana na maafisa wa Msumbiji kumsaka mganga Maheza.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment