Wachezaji wa Hispania Waingizwa Mjini Afrika Kusini

Saturday, July 10, 2010 / Posted by ishak /


Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya soka ya Hispania ambayo itacheza fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili, wameibiwa mali zao walizoziacha kwenye vyumba vya hoteli waliyofikia nchini Afrika Kusini.
Sergio Busquets na Pedro Rodriguez waliibiwa mali zao hotelini wakati Hispania ilipokuwa ikijiandaa kucheza mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mjini Durban.

Vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa vyumba vya wachezaji hao vilivunjwa na wezi walifanikiwa kuondoka na baadhi ya vitu walivyovikuta kwenye vyumba hivyo.

Busquets aliibiwa euro 800 wakati Pedro aliibiwa euro 1,000 zilizokuwa kwenye sefu yake.

"Hakuna mtu anayependa kuibiwa" alisema Busquets.

Shirikisho la soka la Hispania halijasema chochote kuhusiana na wizi huo.

Mwanzoni mwa mechi za fainali za kombe la dunia, wachezaji watatu wa Ugiriki waliibiwa pesa zao walizoziacha kwenye vyumba vyao vya hoteli mjini Durban.

Hispania itacheza na Uholanzi siku ya jumapili katika mechi ya fainali ya kombe la dunia.


source nifahamishe