Kwa mara nyingine tena serikali ya China imekamata tani 64 za maziwa ya watoto ambayo yamechanganywa na kemikali za viwandani ili kufoji ubora wa maziwa. Maziwa hayo yaliua watoto sita mwishoni mwa mwaka juzi na kuwageuza wagonjwa mamia ya watoto.
Maziwa ya watoto yenye sumu ambayo yaliua watoto sita na kuwafanya maelfu ya watoto wawe wagonjwa, yamegundulika tena nchini China.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua la nchini China, tani 64 za maziwa ya watoto ambayo yamechanganywa na kemikali za melamine zinazotumika viwandani, zimegundulika kwenye jimbo la Qinghai nchini humo.
Kemikali za melamine hutumika zaidi kwenye viwanda vya kutengeneza plastiki lakini zinapochangwa na maziwa ya watoto huyafanya maziwa yaonekane yana protini nyingi sana hivyo kuyafanya maziwa hayo yaonekane yana ubora wa hali ya juu na bei yake kuwa juu.
Taarifa iliyotolewa ilisema kuwa waandaaji wa maziwa hayo waliweka kiasi cha melamine mara 500 zaidi ya kiwango kinachokubalika kisheria.
Kemikali ya melamine iliwasababishia watoto waliotumia maziwa hayo kuwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo na figo zao kushindwa kufanya kazi.
Watoto sita walifariki na watoto wengine 300,000 waliugua ghafla na kulazimika kupatiwa matibabu.
Mwezi novemba mwaka jana, watu wawili waliuliwa kwa kudungwa sindano za sumu nchini China kwa kujihusisha na biashara ya kutengeneza na kuuza maziwa hayo ya watoto yenye sumu.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment