Mike Tyson Aenda Makka Kuhiji

Tuesday, July 06, 2010 / Posted by ishak /


Bingwa wa dunia wa zamani wa ndondi, Mike Tyson ambaye alibadili dini kuwa muislamu alipokuwa jela kwenye miaka ya 1990 yupo nchini Saudi Arabia kwaajili ya hija ndogo.
Bingwa wa dunia wa zamani wa ngumi za uzito wa juu, Mike Tyson anatembelea miji mitakatifu ya waislamu Makka na Madina kwaajili ya kuhiji.

Tyson ambaye alikuwa bingwa dunia kuanzia mwaka 1986 hadi 1990, aliwasili Madina siku ya ijumaa akiwa na maafisa wa umoja wa Daa'wa wa Kanada kwaajili ya Umrah ambayo ni hija ndogo.

Baada ya kutoka Madina, Tyson ataenda Makka na gazeti la Okaz la Saudia limeripoti kuwa Tyson ana mpango wa kutembelea pia miji mingine ya Saudia.

Tyson mwenye umri wa miaka 44 alibadili dini kuwa muislamu wakati alipokuwa jela akitumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kumbaka mrembo wa Marekani mwaka 1991. Hata hivyo alitumikia miaka mitatu jela na kuachiwa huru.

Baada ya kutoka jela alijaribu kurudi tena kwenye ngumi lakini hakuweza kulirudia taji lake na mwishoe aliachana na ndondi mwaka 2005.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment