Mwanamke Ajaribu Kufungua Mlango wa Ndege Ikiwa Angani

Thursday, July 08, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja nchini Kanada alisababisha kizaazaa ndani ya ndege iliyokuwa imebeba abiria 131 wakati alipolazimisha kufungua mlango wa ndege huku ndege ikiwa angani.
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Barbara Loretta Morton, 47, alipelekea ndege ibadili mwelekeo wake na kutua kwa dharura baada ya kulazimisha kufungua mlango wa ndege huku ndege ikiwa angani.

Wafanyakazi wa ndani ya ndege ya WestJet ambayo ilikuwa imebeba abiria 131 walitumia nguvu za ziada kumzuia mwanamama huyo asifungue mlango wa ndege, iliripoti televisheni ya CTV News.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Calgary kuelekea Halifax, ililazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Winnipeg.

Barbara alikamatwa na alifunguliwa mashtaka ya kuwashambulia watu, kuhatarisha maisha ya watu na kukataa kufuata maelezo ya wafanyakazi wa ndani ya ndege.

Mfanyakazi mmoja wa ndani ya ndege hiyo na abiria mmoja mwenye umri wa miaka 77 walijeruhiwa katika purukushani hiyo ya kumzuia Barbara asifungue mlango wa ndege.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment