Mtoto wa Miaka 2 Mwenye Kilo 41

Wednesday, March 03, 2010 / Posted by ishak /


Kwa umri ana miaka miwili tu lakini kutokana na unene wake mtoto huyu wa nchini China ana uzito wa kilo 41 na bado anaendelea kunenepa.
Mtoto wa kike Pang Ya wa nchini China ingawa ana umri wa miaka miwili tu ana uzito wa kilo 41.

Uzito wa mtoto Pang ni sawa sawa na uzito wa mwanamke mtu mzima wa nchini China mwenye umbile la wastani.

Wazazi wake wamekuwa wakihangaika kutafuta tiba ya unene wa mtoto Pang ambao unatishia maisha yake.

"Madaktari hawajui nini chanzo cha unene wake hali ambayo inatufanya tuwe na hofu kubwa kuhusiana na maisha yake", alisema baba wa mtoto huyo.

Mtoto Pang ambaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Taocun katika jimbo la Shanxi, alizaliwa akiwa na uzito wa kawaida wa kilo 3.6.

Katika takwimu za serikali ya China zilizotolewa hivi karibuni, watu milioni 60 wa nchini humo wanakabiliwa na matatizo ya unene uliokithiri.

source nifahamishe