Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa

Wednesday, March 03, 2010 / Posted by ishak /


Shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini imeyafunga mabweni yake na kuwalazimisha wanafunzi wote waondoke baada ya wanafunzi 27 wa shule hiyo kugundulika wanaendeleza tabia ya usagaji shuleni hapo.
Maafisa wa elimu wa nchini Afrika Kusini wanafanyia uchunguzi ripoti ya kufungwa kwa mabweni ya shule ya sekondari ya wasichana kutokana na tabia ya wanafunzi wa kike kusagana.

Wanafunzi wawili wa kike walikamatwa wakibusiana na wanafunzi wengine kadhaa inasemekana wako kwenye mahusiano ya jinsia moja.

Jumla ya wanafunzi 27 wamefukuzwa shule kutokana na tabia hiyo ya usagaji.

Watetezi wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini wamekuja juu wakipinga uamuzi wa shule hiyo kwakuwa mahusiano ya jinsia moja yanaruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyoruhusu wasagaji na mashoga kujitawala kama katika nchi za barani ulaya na Amerika.

Wanafunzi waliofukuzwa shule katika shule hiyo iliyopo KwaZulu-Natal hawakutajwa majina yao kwa vyombo vya habari na jina la shule hiyo nalo liliwekwa kapuni.

Gazeti la The Star la nchini humo lilisema kwamba wanafunzi ambao walishindwa kurudi majumbani mwao walipewa hifadhi kwenye nyumba zilizo karibu na shule hiyo.

Msemaji wa kitengo cha elimu cha Afrika Kusini, Sihle Mlotshwa alinukuliwa na gazeti hilo pia akisema kuwa shule hiyo haina haki ya kuwafukuza au kuwasimamisha shule wanafunzi kwasababu ya masuala yao ya kijinsia.

source nifahamishe