'Osama Bin Laden ni Kibaraka wa Marekani' - Fidel Castro

Tuesday, August 31, 2010 / Posted by ishak /


Osama bin Laden ni kibaraka wa Marekani ambaye anatumiwa na serikali ya Marekani kama njia ya kutoa vitisho vyake, hayo yalisemwa na rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro.
Rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro amesema kuwa Osama bin Laden anafanya kazi CIA na alikuwa akitumiwa na rais wa zamani wa Marekani, George Bush kutangaza vitisho vyake duniani.

Castro alisema kuwa wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho kwa nchi yoyote alimtumia Osama bin Laden kama sababu.

Castro alisema kuwa amejua hayo kwakuwa ameona ushahidi wa maandiko uliotolewa na taasisi ya WikiLeaks ambayo imejipatia umaarufu duniani kwa kutoa taarifa za mambo yaliyofanywa siri.

Castro aliyasema hayo wakati akiongea na mwandishi wa habari wa Lithuania, Daniel Estulin, ambaye anajulikana kwa kuzifanyia uchunguzi taarifa zenye utata.

"Osama anafanya kazi chini ya ikulu ya Marekani, Bush alikuwa na sapoti ya Osama wakati wote", alisema Castro.

"Wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho duniani, alitoa hotuba kuhusiana na Bin Laden akimtaja kuwa anafanya mipango kufanya matukio ya kigaidi".

Castro alisema kuwa maelfu ya kurasa za WikiLeaks zimeweka wazi Al-Qaida wanamfanyia nani kazi.

"Aliyetuthibitishia kuwa Bin Laden ni kibaraka wa CIA ni WikiLeaks, wametoa nyaraka za kuthibitisha hivyo", alisema Castro bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusiana na madai yake hayo.

source nifahamishe