Miaka 9 Jela Kwa Kuendesha Gari Huku Akiangalia Ngono

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak /


Dereva wa lori wa nchini Marekani ambaye alikuwa akiendesha lori lake huku akiangalia video za ngono kwenye laptop na kupelekea ajali iliyosababisha kifo cha mtu mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka 9.
Thomas Wallace wa Ohio nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka tisa baada ya kusababisha ajali iliyoua mtu mmoja.

Wallace alikuwa akiendesha lori lake huku akiangalia video za ngono kwenye laptop yake hali iliyopekea kuligonga gari la mlemavu na kupelekea kifo chake.

Mahakama iliambiwa kuwa siku ya tukio hilo disemba 12 mwaka jana, Wallace aliligonga gari la Julie Stratton, mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni mama wa watoto wawili.

Akiongea mahakamani huku akimwaga chozi, Wallace mwenye umri wa miaka 45, aliiomba radhi familia ya marehemu kwa kusababisha ajali hiyo iliyopelekea wapoteze kipenzi chao.

Wallace alihukumiwa kwenda jela miaka 9 ingawa awali ilikisiwa angetupwa jela kati ya miaka mitano na 15.

source nifahamishe