Mmoja wa wachimba madini wa nchini Chile ambao wamenasa mita 700 chini ya ardhi baada ya mgodi wa dhahabu waliokuwemo kuporomoka, ana kesi kubwa ya kujibu nyumbani akifanikiwa kutoka salama kwenye migodi hiyo baada ya mkewe kukutana na kimada wake kw
Mchimba madini wa nchini Chile ambaye amenasa mita 700 chini ya ardhi pamoja na wenzake 32, ana kesi kubwa ya kujibu akitoka salama kwenye migodi hiyo baada ya mkewe kukutana na kimada wake kwenye migodi hiyo.
Taarifa zilisema kuwa mke wa mchimba madini Yonni Barrios alihuzunika baada ya kugundua kuwa mumewe ana kimada na kimada huyo amekuwa akijitangaza kama jamaa wa karibu wa Barrios.
Mke wa Barrios anayeitwa Marta Silanas alisema kuwa alishtushwa sana baada ya kumsikia kimada wa mume wake, Susana Valenzuela akiliita jina la mumewe kwa sauti.
"Barrios ni mume wangu, ananipenda na mimi ni mke wake wa ndoa, huyu mwanamke hatambuliki kisheria", alisikika akisema Marta.
Lakini Susana naye hakukaa kimya, alijibu kuwa alikutana na Barrios miaka mitano iliyopita na wana mpango wa kufunga ndoa baada ya Barrios kuahidi atampa talaka mkewe ili wawe pamoja.
Susana alisisitiza kuwa ataendelea kumsubiria Barrios amuache mkewe.
Barrios na wenzake wamenasa mita 700 chini ya ardhi baada ya mgodi waliokuwemo kuporomoka, wataendelea kukaa huko chini kwa miezi minne zaidi wakati jitihada za kuwaokoa zitakapokamilika.
Kwa sasa wanatumiwa chakula, maji na madawa kupitia mashimo matatu madogo yaliyochimbwa ili kuwapitishia vitu hivyo kwa kupitia kwenye mabomba.
Barrios ni mtu muhimu sana miongoni mwa wachimba madini hao kwani yeye ndiye amekuwa akiwatibu wenzake kutokana na mafunzo ya huduma ya kwanza aliyochukua zamani.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment