Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak /


Mchezaji mashuhuri wa soka la Kimarekani ambaye alijipatia maarufu kwa nywele zake ndefu, amezikatia bima ya dola milioni 1 nywele zake hizo.
Troy Polamalu mwenye umri wa miaka 29 ataendelea kutesa na nywele zake ndefu baada ya kampuni inayotengeneza shampoo za Head and Shoulder ya Procter & Gamble kuamua kuzikatia bima ya dola milioni 1 nywele zake hizo.

Iwapo Troy atakumbana na tukio lolote litakalopelekea apoteze nywele zake, kampuni ya bima italipa fidia zote.

Troy ambaye huichezea timu ya Pittsburg Steelers katika ligi ya NFL ya nchini Marekani ana nywele ndefu sana ambazo zina urefu wa mita moja.

source nifahamishe

Troy mbali ya nywele zake hizo, amejipatia umaarufu mkubwa kwa uchezaji wake wa soka la Kimarekani na amewahi kuchaguliwa kwenye NFL All Star kwa miaka mitano mfululizo.

Hata hivyo nywele zake hizo ambazo amedai amekuwa akizitunza kwa miaka 10 sasa, zimekuwa zikimsababishia matatizo uwanjani kwani baadhi ya wachezaji wa timu pinzani wamekuwa wakizitumia kuzivuta ili kumdondosha chini.