Mtoto Yatima wa Miaka 10 Amuua Mama Aliyejitolea Kumlea

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak /


Mtoto mwenye umri wa miaka 10 wa nchini Thailand ambaye alinusurika kufariki wakati wa tufani la Tsunami nchini humo lililowaua wazazi wake wote wawili, amefunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanamke aliyejitolea kumlea ambaye alikuwa akimbeza kuhusiana
Polisi wa Jakarta Indonesia walimfungulia mashtaka mtoto huyo baada ya kumkuta mwanamke aliyejitolea kumlea Etty Rochyati mwenye umri wa miaka 55, akiwa amefariki baada ya kupigwa na kitu kizito na kuchomwa chomwa na kisu tumboni, limeripoti gazeti la Jakarta Globe .

Maiti ya mwanamke huyo ilikutwa kwenye kiambaza cha nyumba yake akiwa na majeraha mengi kichwani na majeraha ya kisu tumboni mwake.

Mtoto huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu ya umri wake mdogo, aliwaambia polisi kuwa mwanamke huyo alikuwa akimnyanyasa kwa maneno akimwambia “Hujui kuwa wewe huna baba wala mama?” na wakati mwingine alikuwa akitishia kumfukuza nyumbani kwake asipofuata amri zake.

Mtoto huyo alinusurika kwenye gharika la Tsunami lililokiteketeza kijiji chake kwenye kisiwa cha Nias ambapo wazazi wake wote wawili walifariki.

Mtoto huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela iwapo atapatikana na hatia lakini taasisi ya kutetea haki za watoto nchini humo inapigania mahakama imhukumu mtoto huyo kama mtoto na hivyo kutoa adhabu ndogo.

“Kitu alichokifanya mtoto huyu kinaweza kuhesabika kama kitendo cha kujilinda kutokana na manyanyaso na wala hakukusudia kufanya kitendo hiki”, alisema katibu wa taasisi hiyo Arist Merderka Sirait.

“Hapa hatudili na kesi ya mwanaume wa miaka 22, tuna mtoto wa miaka 10 ambaye hajui chochote na ambaye ana maisha marefu baadae”, aliongeza katibu huyo.

Katibu huyo alisema kuwa familia ya mwanamke aliyeuliwa imekubaliana kuifuta kesi dhidi ya mtoto huyo na wapo katika taratibu za kuwasiliana na maafisa wa upelelezi na wanasheria kujua mustakbali wa kesi hiyo.


source.nifahamishe.com

0 comments:

Post a Comment