aliempiga aisha picha asakwa

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak /


Imeelezwa na vyanzo vyetu kuwa Khumalo, aliye raia wa Afrika Kusini, ndiye anayetuhumiwa kumpeleka Aisha nchini humo ambako alimlaghai na kumpiga picha chafu kabla ya kurudi Bongo kuzisambaza.

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka aliliambia gazeti hili kuwa picha hizo za Aisha ambaye ni mwajiriwa wake kwenye Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, zimemfedhehesha na zimemuudhi.
Alisema, tayari analo jibu kamili la mtu aliyehusika na mchezo mzima, hivyo akaahidi kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kabla ya kumuweka ‘ubayani’ kwa kitendo alichofanya.

Asha alisema kuwa kitendo cha Aisha kupigwa picha chafu siyo tu kwamba ni aibu, bali kimeichafua bendi yake kwa sababu ndiyo ambayo mnenguaji huyo anaifanyia kazi.
Aliendelea kusema, Khumalo ni mpenzi wa Aisha na alimpiga picha hizo wakiwa faragha, hivyo haikuwa sahihi kwa raia huyo wa Sauz, kuzisambaza kwa sababu yoyote ile.

“Mimi sijafurahishwa hata kidogo kwa maana ni kitendo cha udhalilishaji, isitoshe huyo ni bwana wake ambaye wapo naye muda mrefu, na ndiye aliyemshawishi kwenda hata huko Afrika Kusini,” alisema Asha a.k.a Iron Lady na kuongeza:
“Nilikuwa naongea sana na huyo Steven Khumalo, hata hapa nina ‘meseji’ zake kwenye simu yangu, na kama sababu ni dawa za kulevya, basi angempiga hizo halafu akazileta ofisini kwangu nimshughulikie kuliko kumpiga za utupu na kusambaza gazetini.”

Asha aliendelea: “Naongea kwa uchungu kama mlezi wa Aisha, pia kama mkurugenzi wake, nitahakikisha Steven namfungulia mashtaka na anakamatwa, asifikiri kwa sababu yeye ni mgeni ndiyo hatuwezi kumkamata.”
Meneja wa Twanga Pepeta, Abuu Semhando alisema kuwa Steven si mtu mwema kwa sababu ndiye aliyemshawishi Aisha kwenda Afrika Kusini ambako amemgeuka na kumpiga picha chafu ambazo amekuja kuzisambaza Bongo.

“Huyo Steven angetuambia sisi kuwa Aisha anavuta bangi nasi tungejua jinsi ya kumsaidia, kuliko alichokifanya kwa sababu kimetudhalilisha,” alisema Abuu a.k.a Baba Diana.
Mnenguaji mwenye jina kubwa Bongo, Lillian Tungaraza ‘Internet’, aliliambia Risasi Mchanganyiko juzi kuwa tangu alipoziona picha za Aisha, ufanisi wake umepungua kutokana na kukosa msisimko wa kazi.

Internet ambaye mashabiki humtambua kama mpinzani halisi wa Aisha jukwaani, alisema kuwa kinachomuumiza zaidi ni kuona kwamba aliyemfanyia hivyo mwenzake ni ‘bwana’ke’ wa muda mrefu.
“Sisi tulijua anakwenda kufanya kazi lakini kumbe amekwenda kumdhalilisha. Mimi naamini hizo dawa alimlisha ili aweze kumnyanyasa na kumdhalilisha,” alisema Lillian Internet.

Gazeti hili lilipompata Khumalo, alisema, anajua kuwa anasakwa na mtu anayemtafuta kwa udi na uvumba ni Asha Baraka, hivyo akasisitiza kwamba haogopi na hakuna wa kumbabaisha.
“Najua Asha Baraka ndiye anayepika kila kitu lakini mimi sibabaishwi. Hizo picha sikupiga mimi, mwenyewe nimeletewa na marafiki zangu ili kunionesha kuwa mchumba wangu hafai.

“Zimeunganishwa tofauti tofauti, sijapiga picha mimi. Kwanza mimi ndiye napaswa kulaumu kuwa nimedhalilishwa, mtu ambaye nilitarajia ningefunga naye ndoa kumbe ni mchafu kiasi hiki,” alisema Khumalo.
Aliendelea kusema: “Hivi sasa simtaki tena Aisha, nimemwambia mama ampe nauli ili arudi huku Bongo, sitaki aendelee kuwepo kule kwa sababu alikuwepo kwa sababu yangu na sasa simtaki aondoke.”

Wakati tunaelekea mtamboni, kuna habari kuwa polisi wamekwishaanza kazi ya kumsaka Khumalo, ingawa halijaelezwa aliyeshtaki ni nani.

source.globulpubliks