OBAMA akutana na wakuu wa usalama wake

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak /


Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mkutano huo, Rais Obama amesema vyombo vya usalama nchini humo vinatambua vitisho vilivyopo vya usalama.

Wakosoaji wamekuwa wakijadili kwamba njama za kufanya mashambulio wakati wa Krismas, zimeonesha udhaifu katika mfumo wa upelelezi nchini humo, ambao ungepaswa kushughulikiwa bada ya kutokea kwa shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 nchini humo.

Wakati huohuo, Ikulu ya Marekani imesema nchi hiyo itasimamisha kuwahamisha wafungwa wengine zaidi kutoka katika gereza la Guantanamo kwenda Yemen.
Rais Obama pia amesisitiza nia yake ya kulifunga gereza hilo la Guantanamo.