Kizimbani Kwa Kumtukana Mama Mkwe Wake

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak /

MWANAMKE Salma Hamisi [28] mkazi wa Magomeni, amefikishwa katika mahakama ya mwanzo Magomeni kwa kosa la kumtukana mama mkwe wake matusi ya nguoni.
Salma alifikishwa mahakamani hapo jana majira ya saa 3 asubuhi, ili kujibu shtaka hilo linalomkabili

Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka, Noel kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Desemba 30, mwaka jana, majira ya jioni huko maeneo ya Magomeni Mwembechai.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alifika kwa mama mkwe wake huyo na kuanza kumtukana matusi ya nguoni ya kumdhalilisha.

Moja ya matusi hayo yaliyobainishwa mahakamani hapo ni pamoja na kumwambia mama huyo kuwa alikuwa anamfatilia maisha yake kama mke mwenzake

Hakimu alipomuuliza mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Asha [56] kama ni kweli alitukanwa matusi na mkwe wake huyo alisema alitukanwa matusi mengi ya kumdhalilisha likiwemo kumwambia kuwa anamtaka mwanae huyo wa kiume na baadae kutaka kumpiga.

Mshitakiwa alipoulizwa alikana na kudai kuwa mama mkwe wake ana matatizo ya kuwafuatilia maisha yake yeye na mume wake hali ambayo inaonekana ni kero kubwa kwake na alikana kutaka kumpiga mama huyo.

Mshitakiwa aliachiwa huru kwa dhamana mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Januari 18 mwaka huu.


source.nifahamishe

0 comments:

Post a Comment