Aibu Kubwa Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Danguro

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak /


Moto uliozuka kwenye danguro la mashoga nchini Uswizi ulisababisha wateja wa danguro hilo wakimbie uchi kunusuru maisha yao.
Mmoja wa wateja wa danguro hilo aliyetajwa na gazeti la Blick la Uswizi kuwa jina lake ni Memeth J, alilazimika kuning'inia kwenye dirisha akiwa uchi huku akificha sura yake wakati akisubiri zimamoto waje kumuokoa.

Tukio hilo lilitokea kwenye danguro moja mjini Basel nchini Uswizi ambapo mashoga hujiuza.

Memeth ambaye anakataa kuwa yeye pia alikuwa mteja wa danguro, alijitetea kuwa alienda kwenye danguro hilo kumtembelea rafiki yake wa miaka 10, Tamilo H ambaye ni shoga anayefanya kazi kwenye danguro hilo.

Memeth aliliambia gazeti la Blick kuwa alikuwa akijirusha na shoga huyo kwenye danguro hilo kabla ya kupitiwa na usingizi na kuzinduka danguro hilo likiwa limeshika moto.

Memeth alilazimika kukimbilia kwenye korido ya danguro hilo huko akiwa uchi lakini huko alikutana na kundi la waandishi wa habari na wapiga picha wakiwa pamoja na zimamoto.

Hali hiyo ilimfanya Memeth akimbilie kwenye dirisha na kuacha makalio yake nje huku akificha sura yake kwa kutumia pazia. Alikubali kuondoka kwenye dirisha hilo baada ya zimamoto kumhakikishia kuwa wataendelea kuificha sura yake.

"Nafikiri ndugu zangu hawatanitambua kwa kuangalia makalio yangu", alisema Memeth akiliambia gazeti hilo.

"Familia yangu haijui kuhusiana na tabia yangu hii ndio maana nimelazimika kuificha sura yangu", alisema Memeth ambaye alisema ana umri wa miaka 33.

source nifahamishe