Ili Kuzuia Watu Kufanya Mapenzi, Miti 6,000 Yakatwa Uingereza

Wednesday, March 24, 2010 / Posted by ishak /


Miti ipatayo 6,000 iliyopo pembeni mwa barabara moja kuu nchini Uingereza imekatwa ili kuwazuia watu kupeana huduma za chap chap.
Miti zaidi ya 6,000 iliyopo pembeni barabara namba A666 katika mji wa Darwen kaskazini masharibi mwa Uingereza imeteketezwa ili kuwazuia watu kufanya mapenzi chini ya miti hiyo.

Miti hiyo iliyochukua eneo la hekta 12 ilikuwa ni maarufu kama kituo cha watu wanaopeana huduma za mapenzi za chap chap.

Miti hiyo iliyopandwa baada ya vita vya pili vya dunia, ilikatwa baada ya maafisa wa manispaa ya mji huo kudai kuwa miti hiyo imezeeka na inaweza ikayaangukia magari yanayopita kwenye barabara hiyo.

Lakini sajenti wa polisi Mark Wilson alisema kuwa miti hiyo ilikatwa kutokana na kuwa kero kwa wapitanjia kutokana na baadhi ya watu kupenda kufanya mapenzi kwenye maeneo ya miti hiyo huku wakionekana wazi.

"Lilikuwa ni tatizo la muda mrefu lililoleta kero kero kubwa sana kwa jamii", alisema sajenti Wilson.

Haijajulikana kama kukatwa kwa miti hiyo kutaleta ufumbuzi wa tatizo hilo la watu kujisevia pembeni mwa barabara hiyo.

source nifahamishe