Babu wa Miaka 96 Amuoa Mwanamke wa Miaka 30

Saturday, March 27, 2010 / Posted by ishak /


Babu mwenye umri wa miaka 96 wa nchini Taiwan amekuwa gumzo nchini humo baada ya kufunga ndoa na mwanamke aliyemzidi miaka 66.
Babu Lin Chung ameweka rekodi ya kuwa bwana harusi mwenye umri mkubwa kuliko wote nchini Taiwan baada ya kufunga ndoa na mwanamke mwenye umri wa miaka 30.

Chung amekuwa gumzo kwenye kitongoji cha Tainan baada ya kumuoa mwanamke huyo anayetoka maeneo ya ukanda wa kati nchini China katika jimbo la Hunan.

Chung ambaye hakuwahi kuoa katika ujana wake, ana watoto wawili aliojitolea kuwalea tangia walipokuwa wadogo ambao hivi sasa mmoja kati ya watoto hao ana umri wa miaka 68.

Chung anadai kwamba miaka mitatu iliyopita, alipewa maelezo na Mungu aende kwenye jimbo la Hunan nchini China ili kumtafuta mwanamke anayekuja kuwa mke wake.

Chung alifunga ndoa na mwanamke huyo hivi karibuni pamoja na upinzani mkali toka kwa mwanae huyo wa kujitolea ambaye alikuwa akimuona babu huyo kama amelaghaiwa.

"Inanibidi niwe na mwenza katika uzee wangu... sikuwahi kuwa na mke, kwanini hivi sasa hataki mimi nioe", alisema Mzee Chung.

Chung hivi sasa anashughulikia taratibu za kisheria kumwezesha mkewe ahamie Taiwan toka China ili waishi pamoja.

source nifahamishe