Mtu Mfupi Kuliko Wote Duniani Afariki Dunia

Tuesday, March 16, 2010 / Posted by ishak /


He Pingping mbaye alikuwa kitambulika kama mwanaume mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 74.61 amefariki dunia jumamosi kutokana na matatizo ya moyo.
He Pingping, amefariki dunia nchini Italia akiwa na umri wa miaka 21.

He alikuwa nchini Italia kwaajili ya kushiriki kwenye shoo ya kwenye luninga lakini alisumbuliwa na maumivu makali kwenye kifua na alipowahishwa hospitali wiki mbili zilizopita alifariki siku ya jumamosi kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni matatizo ya moyo.

He alizaliwa nchini China akiwa na ugonjwa unaomfanya awe mfupi sana. Baba yake He Yun aliwahi kusema kuwa He alipozaliwa alikuwa mdogo sana kiasi cha kuenea kwenye viganja vyake vya mikono.

He alitambulika rasmi kama mtu mfupi duniani na kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia, Guinness mnamo mwaka 2008.

Akiwa na taji lake hilo, He alisafiri nchi mbalimbali duniani kutangaza rekodi yake hiyo akiwa na watu wengine waliovunja rekodi za dunia.

Mwezi septemba mwaka 2008, He alienda mjini London, Uingereza na kupiga picha na mwanamke mwenye miguu mirefu kuliko wanawake wote duniani, Svetlana Pankratova.

Mwanzoni mwa mwaka huu, He alisafiri kwenda Istanbul,Uturuki ambapo alikutana na mtu mrefu kuliko wote duniani Sultan Kosen mwenye urefu wa sentimeta 246.5.

Guinness World Records wamesema kuwa mrithi wa taji la He atatangazwa katika siku zijazo.

Hata hivyo, Khagendra Thapa Magar, 18, toka Nepal ndiye anayeonekana kuwa mtu atakayenyakua taji hilo kwani ni mfupi kuliko He akiwa na urefu wa sentimeta 51 tu.

source nifahamishe