Mwanamke Ajitesa Ili Avunje Rekodi ya Dunia

Tuesday, March 16, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke ambaye alivunja rekodi ya dunia kwa kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani kujifungua mtoto, anakula chakula cha kuwatosha wanawake sita kila siku ili aweze kuvunja rekodi ya dunia ya kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani.
Donna Simpson,toka New Jersey,Marekani hivi sasa ana uzito wa kilo 273 lakini ametangaza nia yake ya kula sana ili uzito wake ufikie kilo 450 ndani ya miaka miwili.

Donna ambaye ana umri wa miaka 42 tayari anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani kujifungua mtoto. Alijifungua mtoto wa kike mwaka 2007 wakati huo akiwa na uzito wa kilo 241.

"Ningependa kutimiza kilo 450... ingawa ni vigumu, kumkimbiza kimbiza mtoto wangu kunanifanya nisiongezeke uzito kwa kasi", alisema Donna alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Daily Mail la Uingereza.

Donna ambaye anahitaji scotter kumwezesha kutembea, hula kiasi kikubwa cha chakula kila siku ambacho kingeweza kuwatosha wanawake sita.

Donna ambaye anapewa kampani na mumewe kutimiza rekodi hiyo, hujitahidi asitembee umbali mrefu ili kalori za vyakula anavyokula zisipotee.

Donna anatumia dola 815 kila wiki kwaajili ya kununulia chakula. Donna hujiingizia pesa anazotumia kwa matumizi yake kwa kutumia tovuti yake aliyoifungua ambapo wanaume hulipa pesa kumuangalia yeye akifakamia vyakula vyake.

source nifahamishe