Mgonjwa wa Kifafa Ala Ubongo wa Mtoto Akidai ni Tiba ya Kifafa

Friday, March 19, 2010 / Posted by ishak /

Mwanaume mmoja nchini China anashikiliwa na polisi baada ya kumuua mtoto wa miaka 11 na kisha kuula ubongo wake akidai kuwa aliambiwa kuwa tiba ya kifafa ni ubongo wa mtoto.
Polisi nchini China wanamshikilia mwanaume aliyemuua mtoto wa miaka 11 na kisha kuula ubongo wake akidai kuwa mke wake wa zamani aliwahi kumwambia kuwa ubongo wa mtoto ni tiba bora ya ugonjwa wa kifafa.

Wang Chaoxu, wa kijiji cha Qixian katika jimbo la Yunnan, kusini mwa China alitiwa mbaroni jumatano baada ya polisi kukuta mwili wa mtoto wa kiume wa miaka 11, Li Xuetang ukiwa umezikwa kwenye kichaka.

Kichwa cha mtoto huyo kilikuwa kimepasuliwa na sehemu ya ubongo wake ilikuwa imenyofolewa.

Mama wa mtoto huyo, Yu Chaohu alisema kuwa alipatwa wasiwasi mkubwa baada ya mtoto wake kutoweka ghafla majira ya jioni.

"Giza lilikuwa likiingia na sikuweza kumuona mtoto wangu, niliwaomba wanakijiji wanisaidie kumtafuta na hata nilimuomba mkuu wa kijiji apeleke tangazo redioni", alisema mama wa mtoto huyo kwa uchungu.

Mama wa mtoto Li hakuruhusiwa kuiona maiti ya mwanae kutokana na jinsi ilivyokuwa imeharibika vibaya sana.

Wakati Wang alipotiwa mbaroni alisema kuwa alikuwa akiamini kuwa kwa kula ubongo wa mtoto uliochangwanya na minyoo na sisimizi, ugonjwa wake wa kifafa ungeondoka.

Polisi pia wanaendelea kufanya uchunguzi kujua kama Wang anahusika na kifo cha mtoto wa kike wa miaka mitatu ambaye mwili wake ulipatikana siku hiyo hiyo huku kichwa cha mtoto huyo nacho kikiwa kimepasuliwa na ubongo wake ukiwa umenyofolewa

source nifahamishe