Migahawa Kupigwa Marufuku Kuweka Chumvi Kwenye Chakula

Sunday, March 14, 2010 / Posted by ishak /


Wapishi katika jiji la New York nchini Marekani wako kwenye hatihati ya kupigwa faini ya dola 1,000 iwapo wataweka chumvi kwenye vyakula wanavyopika.
Manispaa ya New York imepokea muswada wa sheria ambao utawapiga marufuku wapishi kwenye migahawa yote ya mjini humo kuweka kiasi chochote kile cha chumvi kwenye vyakula wanavyoviandaa.

Muandaaji wa muswada huo Felix Ortiz alisema kuwa muswada huo ukipitishwa itakuwa ni hatua nzuri sana ya kuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaofariki kutokana na magonjwa ya moyo.

Muungano wa wapishi wa New York umeupinga muswada huo na kuuita ni wa kipuuzi.

Tom Colicchio, mmiliki wa mgahawa wa Craft ambaye pia ni nyota wa mapishi kwenye televisheni za Marekani alisema "Iwapo watapiga marufuku chumvi kwenye chakula, hakuna atakayekuja hapa kula".

Kwa mujibu wa muswada huo, Migahawa haitaruhusiwa kuweka kiasi chochote cha chumvi kwenye vyakula vyao lakini chumvi itawekwa kwenye meza kwa mteja kujiwekea mwenyewe.

Jumla ya wakazi milioni 1.5 wa New York wanakabiliwa na matatizo ya moyo na shinikizo la damu.

Inakakadiriwa kuwa hatua ya kupunguza matumizi ya chumvi itasaidia kuokoa maisha ya watu 100,000

source nifahamishe