Sura ya Yesu Yadaiwa Kuonekana Kwenye Kikaangio

Monday, March 15, 2010 / Posted by ishak /


Picha yenye sura ya Yesu imedaiwa kuonekana kwenye kikaangio cha mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye aliunguza mapishi yake ya nyama ya nguruwe kwenye kikaangio hicho wakati alipopitiwa na usingizi wakati anapika.
Toby Elles, 22, anadai kugundua sura ya Yesu kwenye kikaangio baada ya kuunguza chakula alipopitiwa na usingizi wakati anapika.

Toby anadai kuwa baada ya kuziokoa nyama zake za nguruwe ambazo zilikuwa zikiungua kwenye kikaangio hicho, hakuamini macho yake alipoona sura kama ya Yesu kwenye kikaangio.

"Sura yake inaonekana wazi, pua, macho na ndevu zake zote zinaonekana wazi", alisema Toby.

"Nilipitiwa na usingizi wakati nakaanga nyama ya nguruwe, iliungua na ndipo sura hii ya Yesu ilipotokea, ni kama miujiza vile", alisema Toby mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Halifax nchini Uingereza.

Toby anasema kwamba hatakiosha kikaangio hicho na badala yake atakiweka ukutani kimlinde yeye na nyumba yake.

"Nafikiria kutengeneza fremu ya kioo nikiweke hiki kikaangio, kimekuwa gumzo kwa kila anayeingia nyumbani kwangu".


source nifahamishe