Aiba Mguu wa Maiti toka Kaburini

Tuesday, May 11, 2010 / Posted by ishak /


Kijana mmoja wa Kimarekani ametiwa mbaroni na polisi baada ya kuiba mguu wa maiti ya msichana wa kiyahudi toka kwenye makaburi ya wayahudi nchini Marekani.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyetambulika kwa jina la Daniel Wayne Staley, alitiwa mbaroni ijumaa alfajiri akiwa ameubeba mguu wa binadamu aliouiba toka kwenye makaburi ya wayahudi mjini Dallas.

Polisi waliwasili kwenye eneo la tukio majira ya saa tisa na nusu usiku baada ya kupewa taarifa na mtu aliyeshuhudia tukio hilo.

Daniel alikamatwa akiwa amebeba mfuko wa rambo ambao ndani yake kulikuwa na mguu wa binadamu.

"Nilifukua kaburi na kuuchukua mguu wa maiti ya msichana ya kiyahudi kwakuwa nilikuwa nikitaka mguu", Daniel aliwaambia polisi.

Daniel amefunguliwa mashtaka ya wizi wa maiti ya binadamu na huenda akatupwa jela mwaka mmoja na kupigwa faini ya dola 4,000, limeripoti gazeti la The Dallas Morning News.

Daniel hakusema mguu huo alikuwa akiuhitaji kwa shuguli zipi.

source nifahamishe