Nani Kasema Mapenzi Hayana Umri?

Sunday, May 09, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mwenye umri wa miaka 28 wa nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kutumia fimbo ya kutembelea ya mpenzi wake mwenye umri wa miaka 77 kumtandika nayo na kumjeruhi vibaya sana.
Kristina N. Pongracz mwanamke mwenye umri wa miaka 28 wa Bedford County, Virginia nchini Marekani anashikiliwa na polisi kwa kumjeruhi mpenzi wake babu mwenye umri wa miaka 77.

Babu William Herchenrider alikutwa nyumbani kwake kwenye dimbwi la damu akiwa amejeruhiwa vibaya sana huku mkongoja wake ukiwa pembeni.

Taarifa zilisema kuwa Kristina alitumia mkongoja wa babu William kumtandika nao na kumjeruhi vibaya sana kabla ya kuanza kunywa pombe na kupitiwa na usingizi pembeni yake.

Polisi walifika kwenye eneo la tukio baada ya kupewa taarifa za kelele toka kwenye nyumba ya babu William.

William aliwahishwa hospitali kupatiwa matibabu huku mpenzi wake akitupwa mahabusu kwenye jela ya Blue Ridge mjini Bedford.


source nifahamishe